Dodoma. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na mijadala inayoendelea bungeni ya kumlinganisha na mtangulizi wake, hayati John Magufuli.
Akizungumza leo Jumapili Aprili 18, 2021 katika kongamano la viongozi wa dini, Samia amesema yeye na Magufuli ni kitu kimoja na anaendeleza kazi iliyofanywa na mtangukizi wake huyo aliyefariki dunia Machi 17, 2021 kwa ugonjwa wa moyo.
“Inasikitisha sana kuona watu wanapiga ngoma mitandaoni na inachezwa bungeni. Tena inachezwa kwa umaridadi."
“Mmejikita kulinganisha watu badala ya ajenda, mnalinganisha Magufuli na Samia. Hawa watu ni kitu kimoja, nimekuwa nikifuatilia mijadala yenu bungeni haina afya kwenye Taifa, jikiteni kwenye bajeti za wizara mbalimbali mengine tutayajadili mbeleni, " amesema.
Post a Comment