Dkt. Philip Mpango alithibitishwa kama Makamu wa Rais wa Tanzania, Machi 30, 2021

   Dkt. Philip Mpango, ambaye ameapishwa leo kama makamu wa rais wa Tanzania, ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango katika Serikali ya Awamu ya Tano, amehudumu katika wizara hiyo kwa muda wa miaka takribani sita.



Philip Mpango ni nani?

Dkt. Mpango ni mzaliwa wa Kigoma, baba yake ni marehemu Isidori Nzabhayanga Mpango, ambaye alizaliwa katika Kijiji cha Kasumo, Wilaya ya Kasulu.

Dkt. Mpango alizaliwa huko Kasumo pia,  na ni kaka mdogo wa Askofu mstaafu wa Jimbo la Anglikana la Tanganyika Magharibi - Kasulu katika mkoa wa Kigoma, Dkt. Gerard Mpango.

Dkt. Mpango ni mchumi na shahada ya uzamili ya uchumi.

Kuanzia 1990 hadi 2000, alifanya kazi kama mhadhiri mwandamizi wa uchumi katika Kitivo cha Biashara (sasa Shule ya Biashara) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Alikuwa akifundisha "Microeconomics", "Macroeconomics" (kwa mwaka wa pili) na "Fedha za Umma" kwa mwaka wa tatu na kozi za uzamili. (Uchumi mdogo, Uchumi Mkubwa na Maswala ya Fedha za Umma.)

Aliwahi kuwa Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Mkuu wa Kamati ya Ushauri ya Kiuchumi wakati huo, katibu binafsi wa Rais Jakaya Kikwete wa maswala ya uchumi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, kabla ya kuhamishiwa kwa Tume ya Mipango, Ofisi ya Rais.

Alishika nyadhifa hizi zote wakati wa utawala wa Kikwete.

Wakati Hayati Magufuli alipoingia madarakani alimteua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na siku chache baadaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.




Katika uchaguzi wa 2020 alishinda kiti cha ubunge jimbo la Buhingwe.

Kisha akateuliwa tena kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Dkt. Mpango huwa hana tabia za kawaida ambazo unaweza kuzihusisha na wanasiasa wa Kiafrika. Dkt. Mpango ni mkweli, mwenye haki, mcha Mungu na yule anayeamini katika matendo badala ya maneno.

Sababu hizo, pamoja na uwezo wake kama mchumi, ndizo zilizomfanya awe Waziri wa Fedha kwa miaka sita yote ya utawala wa Rais Magufuli.

Hili sio jambo dogo kwa sababu wizara ilikuwa ikifuatiliwa kwa karibu na Rais Magufuli ambaye alikuwa anajulikana kwa kutowavumilia wateule wake ambao walionekana kutotimiza matarajio yake.

Uchaguzi mkuu wa 2020 ulikuwa mara yake ya kwanza kugombea ubunge - bila shaka bila kungojea tena uteuzi wa Rais Magufuli.




Uteuzi wake kuwa makamu wa rais wa tanzania,

Bunge lilithibitisha Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwasilisha uteuzi wake wa makamu wa rais katika kikao maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) .

Jina hilo baadaye liliwasilishwa bungeni na kupitishwa kwa kura 363 sawa na asilimia 100 ya kura zote zilizopigwa.

Baada ya kupokea jina lake, Spika Job Ndugai alitangaza bungeni jina lililopendekezwa na Rais Samia.

Mara tu baada ya tangazo hilo, bunge lilipiga makofi.

Bwana Mpango alikuwa waziri mwandamizi katika serikali ya marehemu John Magufuli akihudumu kama waziri wa fedha.

Na kulingana na Katiba ya Tanzania, 50% ya wabunge wanahitajika kukubali uteuzi wa uthibitisho.

Kabla jina hilo kuwasilishwa bungeni leo, liliwasilishwa kwanza kwa Kamati Kuu ya CCM na kupitishwa.

"Nimepigwa na butwaa"

Mara tu jina lake liliposomwa, Spika Ndugai alimpa Dkt. Mpango muda wa kujieleza Bungeni.

Dkt. Mpango alisema kwamba hakujua chochote juu ya uteuzi huo na kwamba alikuwa amepigwa na butwaa.



'' ... Hii ni heshima kubwa, sikuwahi kuota kama nitaipata ... Hadi Naibu Waziri wangu alipojibu maswali asubuhi ya leo, nilikuwa nikifikiria juu ya majukumu yangu yanayonikabili ikiwa ni pamoja na mishahara ya wabunge ambayo baadhi yao imecheleweshwa hadi leo asubuhi. Nimeshangaa ... "

Post a Comment

Previous Post Next Post