Kutana na Isa Hamis ambaye ni kijana anayejushughulisha na kazi ya ukondakta kwa miaka 8 Jijini Arusha, pamoja hayo amewahi kufanya kazi kwenye mashamba ya mpunga yaliyompa uzoefu na uwezo wakutumia sauti yake kuigiza milio ya ndege mbalimbali zaidi ya kumi.

Hamis anasimulia >>”Wakati natoka shuleni tulikuwa na mashamba ya Mpunga maeneo ya Makumira kwa chini, kulinda ndege nafahamu sababu kuna kipindi unaweza kukaa asubuhi mpaka jioni na chakula ukaletewa hukohuko hii ikanifanya nijikute nalia kama ndege”-Hamis

Post a Comment

Previous Post Next Post