fulltim pic
By Saddam Sadick

Shinyanga. Licha ya kukaa muda mrefu nje ya uwanja, lakini haikuharibu chochote kwa staa wa Simba, John Bocco kuendeleza pale alipoishia katika suala la ufungaji mabao na kuwapa raha mashabiki wa timu hiyo.

Bocco akiiongoza timu yake katika dakika 45 za kipindi cha pili dhidi ya wenyeji Mwadui katika dimba la Kambarage mjini Shinyanga, hakutumia muda mrefu kuipatia bao la kwanza akiunganisha kwa kichwa mpira wa Onyango na kuujaza wavuni.

fulltime pic 2

Nahodha huyo aliingia dakika ya 45 na kuongeza nguvu safu ya ushambuliaji akiungana na Kagere ambapo dakika ya 66 aliweza kufunga bao.

fultime pic4

Bao hilo linakuwa la 10 kwa Straika huyo na kuifanya Simba kurudi nafasi ya pili kwa pointi 52 wakiwashusha Azam wenye alama 50 nafasi ya tatu.

ADVERTISEMENT
HALFTIME PIC1

Mwadui walipambana kwa uwezo wao huku wakitumia zaidi nidhamu ya mchezo na kuzuia hatari muda wote na kuwanyima mianya ya kupenya wapinzani.

Hata hivyo dakika ya 67 Kagere aliikosesha bao timu yake baada ya mpira wake kuondoshwa ukiwa unaelekea wavuni huku mashabiki wakiwa tayari wameshasimama kushangilia.

HALFTIME PIC2

Mwadui walibadilika kuanza kushambulia kwa kushtukiza na dakika ya 80 Anicet Revocatus alipiga shuti ambalo lilitoka nje ya lango.

HALFTIME PIC3

Mabadiliko mengine aliyofanya Gomes ni kumtoa Bwalya na nafasi yake kuchukuliwa na Mzamiru Yassin huku Morison akikumbana na kadi ya njano baada ya kile kilochosemekana kuwa kumtolea maneno mwamuzi.

Post a Comment

Previous Post Next Post