Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba anataka kulipwa uero 500,000-kwa-wik i kusaini mkataba mpya na Manchester United, huku Real Madrid, Paris St-Germain na Juventus wakipewa masharti hayo ikiwa wanamtaka kumsajili nyota huyo aliye na umri wa miaka 28. (Star on Sunday)
Chelsea itamenyana na Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumsajili mchezaji wa safu ya kati na nyuma wa Real Madrid na Ufaransa Raphael Varane, 27. (Bild journalist Christian Falk on Twitter)
Tetesi "zimezidi kuongezeka" huko Tottenham kwamba meneja Jose Mourinho hatakuwepo kwenye klabu msimu ujao, Spurs ikijitahidi kupata nafasi ya Ligi ya Mabingwa 2021-22. (Football London)
Wolves wanataka kumuuza winga wa Uhispania Adama Traore ilikuchangisha fedha za kumsajili mchezaji mpya na £30m huenda ikatosha kufanikisha mpango wa usajili wa klabu hiyo . (Football Insider)
Mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling, 26,kwa mra nyingine tena ananyatiwa na Real Madrid, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa England akikakamua kuwa katika kikosi cha kwanza cha soka wiki za hivi karibuni. (Star on Sunday)
Tottenham wanaendelea kumfuatilia mchezaji Emerson,22, wa Brazil, ambaye yuko Real Betis kwa mkopo kutoka Barcelona. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Kiungo wa kati wa Liverpool Georginio Wijnaldum, 30, anapanga kujiunga na Barcelona msimu huu wa joto kwasababu anataka kucheza pamoja na Lionel Messina mwenzake wa Uholanzi Memphis Depay. (Sunday Mirror)
Aston Villa na Crystal Palace wanataka kusaini kiungo wakati wa Chelsea na England Ruben Loftus-Cheek,25, ambaye yuko Fulham kwa mkopo . (Teamtalk)
Post a Comment